Form Five Selection 2025 na Vyuo Vya Kati Tanzania – Taarifa Muhimu
Form Five Selection ni Nini?
Form Five Selection ni mchakato rasmi wa serikali unaowachagua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne kujiunga na Kidato cha Tano au vyuo vya kati mwaka 2025. Mchakato huu unasimamiwa na:
- TAMISEMI
- Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
- NACTVET
Wanafunzi waliofaulu mtihani wa NECTA CSEE 2024 huchaguliwa kwa kuzingatia ufaulu na vipaumbele vya kozi walivyochangua kupitia mfumo wa Selform.
Lengo la Uchaguzi wa Kidato cha Tano na Vyuo 2025
Lengo kuu ni kuwawezesha wanafunzi waliopata ufaulu kuendelea na:
- Masomo ya Sekondari ya Juu (Kidato cha Tano na Sita)
- Mafunzo ya ufundi katika vyuo vya kati vilivyosajiliwa na NACTVET
Vigezo vinavyotumika:
✅ Matokeo ya Kidato cha Nne (NECTA 2024)
✅ Mapendekezo ya mwanafunzi kwenye mfumo wa Selform
✅ Uwezo wa shule au chuo kupokea wanafunzi
Mchakato wa Uchaguzi wa 2025 – Hatua kwa Hatua
- NECTA hutangaza matokeo ya Kidato cha Nne
- Wanafunzi hujaza au kurekebisha tahasusi kupitia Selform
- Serikali hupanga wanafunzi kulingana na ufaulu na vipaumbele
- Orodha ya waliopangiwa hutolewa kwenye tovuti za serikali
Wanafunzi wenye alama za juu hupangiwa shule za kitaifa kama:
- Ilboru
- Kilakala
- Mzumbe
- Tabora Boys
- Tabora Girls
Wengine hupangiwa shule za bweni au kutwa kulingana na matokeo.
Tarehe ya Matokeo ya Form Five Selection 2025
Kwa mujibu wa historia, majina yanatarajiwa kutangazwa Mei 2025.
Mwaka uliopita, 2024, orodha ilitangazwa 30 Mei 2024 kwenye tovuti ya TAMISEMI.
Namna ya Kuangalia Majina ya Kidato cha Tano 2025
Fuata hatua hizi kwenye tovuti ya TAMISEMI:
- Fungua www.tamisemi.go.tz
- Bonyeza link ya Form Five First Selection 2025
- Chagua mkoa uliosoma
- Chagua halmashauri yako
- Tafuta shule uliyosoma
- Angalia jina lako kwenye orodha
- Pakua fomu za kujiunga na ufuate maelekezo
Namna ya Kuangalia Selection kwa Vyuo vya Ufundi (NACTVET) 2025
NACTVET hutangaza orodha kupitia tovuti rasmi:
👉 www.nactvet.go.tz
Utaratibu:
- Tembelea tovuti ya NACTVET
- Chagua aina ya chuo
- Tafuta kwa kutumia mkoa au jina la chuo
- Angalia kama umechaguliwa
Ushauri Muhimu kwa Wanafunzi
📌 Hakikisha taarifa zako kwenye Selform ni sahihi
📌 Tembelea mara kwa mara tovuti za TAMISEMI na NACTVET
📌 Wasiliana na walimu wa shule au viongozi wa elimu kwa msaada