Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania 2025

Pata taarifa za kuripoti na utaratibu wa mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania 2025. Jifunze hatua za kujiunga na huduma rasmi kwa urahisi.

Waraka kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania 2025

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kwa ajili ya kuanza mafunzo ya awali kwa tarehe na utaratibu ufuatao:

  1. Tarehe ya Kuripoti Shule ya Polisi Moshi
    Vijana wote wanapaswa kuripoti kuanzia tarehe 12 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi. Mtu yeyote atakayewasili baada ya tarehe 14 Juni 2025 hatapokelewa na atachukuliwa kuwa amejiuzulu kwenye mafunzo.
  2. Utaratibu wa Safari kwa Kanda na Mikoa
    a) Vijana waliotakiwa usaili Dar es Salaam (Vikosi vya Makao Makuu)
    Watakutana tarehe 12 Juni 2025 saa 12:00 asubuhi katika Uwanja wa Gwaride, Kambi ya Polisi Kilwa Road, kuanza safari ya pamoja kuelekea Moshi.

b) Vijana wa Mikoa ya Tanzania Bara
Wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa walikofanyiwa usaili tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi kwa maelekezo ya safari.

c) Vijana wa Zanzibar (Unguja na Pemba)
Wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi kwa maelekezo ya safari.

  1. Vifaa Muhimu vya Kuambatana Navyo
    Vijana wote wanapaswa kufika Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:
  • Vifaa vya Mavazi na Malazi:
    • Traki suti ya bluu yenye ufito mweupe
    • Fulana nyeupe isiyo na maandishi
    • Raba na soksi nyeusi
    • Bukta mbili za rangi ya bluu
    • Sanduku la chuma (tranka) la bluu
    • Chandarua cheupe cha duara
    • Shuka 4 za bluu mpauko (jozi mbili)
    • Pasi ya mkaa
    • Blanketi moja la kijivu (lisilo na maua wala duvet)
  • Vifaa vya Chakula:
    • Kikombe cha plastiki (cream light)
    • Sahani moja ya chuma (steel dish plate)
  • Vifaa vya Usafi:
    • Sururu moja yenye mpini
    • Ndoo ndogo mbili
    • Fagio la chelewa
  • Vinginevyo:
    • Kadi ya NHIF au Tsh. 50,400/= kwa wasio na bima
    • Vyeti halisi vya taaluma na cheti halisi cha kuzaliwa
    • Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa taifa (NIDA)
    • Nakala za NIDA za wazazi au watu wa karibu (baba, mama, babu, nk.)
    • Picha ndogo za pasipoti 6 (background ya bluu)
    • Nakala 5 za kila cheti kilichoainishwa
    • Fedha za kujikimu
  1. Marufuku ya Simu za Mkononi
    Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni. Mwanafunzi yeyote atakayekutwa na simu atafukuzwa mafunzo mara moja. Shule itatoa utaratibu wa mawasiliano.
  2. Orodha ya Majina
    Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa na inapatikana kupitia kiungo rasmi cha Jeshi la Polisi:
    TANGAZO_LA_KURIPOTI_SHULE_YA_POLISI_MOSHI.pdf

Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Makao Makuu ya Polisi
S.L.P 961, DODOMA
01 Juni 2025