Matokeo ya Darasa la Saba Dar es Salaam 2024

Mkoa wa Dar es Salaam ni kitovu cha biashara na uchumi nchini Tanzania. Pia, sekta ya elimu hapa ni muhimu sana. Kila mwaka, wanafunzi wa darasa la saba kutoka shule takribani 663 za msingi mkoani humaliza Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) unaosimamiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Matokeo ya mtihani huu ni hatua muhimu kwa wanafunzi na wazazi kwa kupanga elimu ya baadaye.

Katika makala hii, nitakuonyesha jinsi ya kuangalia matokeo ya darasa la saba mwaka 2024/2025 mkoa wa Dar es Salaam kwa njia rahisi kupitia tovuti rasmi ya NECTA.

Jinsi ya kuangalia matokeo ya darasa la saba Dar es Salaam 2024:
Fungua tovuti ya NECTA (www.necta.go.tz), bofya sehemu ya “Matokeo,” chagua “Matokeo ya Darasa la Saba,” tafuta mwaka 2024, chagua mkoa wa Dar es Salaam, kisha chagua wilaya na shule unayotaka kuona matokeo yake.


Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba Mkoa wa Dar es Salaam Kupitia Tovuti ya NECTA

Ili kuona matokeo, tembelea tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwenye www.necta.go.tz. Fuata hatua hizi:

  1. Nenda kwenye sehemu ya “Matokeo” kwenye menyu kuu.
  2. Chagua “Matokeo ya Darasa la Saba (PSLE Results)” kutoka kwenye orodha ya matokeo.
  3. Tafuta mwaka wa mitihani, mfano 2024.
  4. Chagua mkoa wa Dar es Salaam.
  5. Chagua wilaya unayotaka kuona matokeo yake (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, au Kigamboni).
  6. Matokeo ya shule zote za msingi katika wilaya hiyo yataonekana, na unaweza kuchagua shule husika kuona matokeo ya wanafunzi.

Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya Zote za Mkoa wa Dar es Salaam

Mkoa wa Dar es Salaam una wilaya tano kuu: Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, na Kigamboni. Kila wilaya ina shule nyingi za msingi zinazoshiriki mtihani huu. Kwa kufuata hatua zilizotajwa, unaweza kupata matokeo kwa kila wilaya kwa urahisi.


Taarifa Muhimu

Matokeo haya yanapatikana tu kupitia tovuti rasmi ya NECTA, kwa sababu hii ni njia salama na ya kuaminika. Tafadhali epuka tovuti zisizo rasmi ili kuepuka udanganyifu. Kwa usalama wa taarifa zako binafsi, hakikisha hutumiishi maelezo yako kwa tovuti isiyo rasmi.