Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na JKT 2025
Majina ya waliochaguliwa JKT 2025 yametoka. Ni wanafunzi wa kidato cha sita. Angalia masharti na majina hapa.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hupokea na kufundisha vijana kwa ajili ya ulinzi wa taifa, uzalendo, na ujasiriamali. Mafunzo haya hujumuisha kilimo, ufugaji na biashara. Ratiba hutolewa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Yaliyomo:
- Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2025
- Vijana wa Mujibu wa Sheria
- Masharti ya Kujiunga na JKT
- Angalia Majina Hapa
Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2025
Vijana wa Mujibu wa Sheria
Hawa ni wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kutoka Tanzania Bara. Wanajiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ya nchi. Hudumu kwa miezi mitatu.
Masharti ya Kujiunga kwa Vijana wa Mujibu wa Sheria
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 35
- Awe amemaliza kidato cha sita au zaidi
- Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi
- Asivute bangi au kutumia dawa za kulevya
- Asipate mimba akiwa jeshini
- Asiwe mtoro (mkataba utaongezwa kwa kosa la utoro)
- Awe na tabia njema
Utaratibu wa Kuchagua Majina
Kila mwaka, JKT huandikisha vijana wa kujitolea kutoka mikoa yote. JKT hutuma barua kwa wakuu wa mikoa wakionyesha idadi ya nafasi. Mkoa hugawa nafasi hizo kwa wilaya, kisha kwa tarafa, kata, na vijiji.
Tangazo la nafasi huwekwa kwenye mbao za matangazo za wilaya.
Usaili
Usaili wa awali hufanywa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya. Kisha usaili wa mkoa hufanyika. Baada ya hapo, timu kutoka Makao Makuu ya JKT hukagua waliochaguliwa.
Vijana hupimwa afya na kusafirishwa kwenda vikosi vya JKT.
👉 ANGALIA HAPA MAJINA